Wednesday, May 9, 2012

TAVA NATIONAL VOLLEYBALL COACHES PROGRAM FOR SECONDARY AND PRIMARY SCHOOL SPORTS TEACHERS.

Shirikisho la mpira wa wavu la Taifa TAVA linaendesha mpango wa maendeleo wa mpira wa wavu nchini kwa kuendesha mafunzo ya ndani ya mchezo huo kwa makocha ambao ni waalimu wa michezo wa shule za msingi na sekodari nchini. Mpango huo wenye jina la mradi hapo juu umefadhiliwa na shirikisho la dunia la mpira wa wavu FIVB katika mfuko wake wa maendeleo. ( FIVB DEVELOPMENT FUND). TAVA imefadhiliwa na mfuko huo, vifaa vyenye jumla ya thamani zaidi ya sh.Milioni 140 vikiwemo mipira na net za kuchezea.

Kupitia mradi huo uliobuniwa na TAVA, TAVA itaendesha mafunzo hayo karibu katika mikoa yote ya Tanzania kwa kuanzia na mikoa kumi ya awali ambayo ni Dar, Tanga,Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Morogoro, Dodoma, Kagera na Zanzibar. Mafunzo hayo tayari yameshafanyika Zanzibar na sasa yanaendelea Tanga na Manyara. Lengo nikufikia zaidi ya waalimu 600 ambao kila mwalimu akifundisha vijana 20 basi zaidi ya vijana 10,000 watakuwa wamenufaika na Mradi huu.

Lengo hasa la TAVA ni kuwa na msingi mzuri wa wachezaji wa baadae hapa nchini. Ni ukweli usiofichika kuwa ni kupitia shule za msingi na sekondari ndipo vipaji vya mchezo wetu uvumbuliwa. Hivyo kwa kuzingatia hilo ni matarajio yetu makubwa kuwa miaka ya mbeleni tutakuwa na wachezaji wengi wazuri waliotoka katika mikono ya waalimu waliopitia mafunzo yetu.

Lengo lingine la TAVA ni kuanzisha na kuimarisha vyama vya mikoa kwa kuwasaidia vifaa vyama vyote vilivyo hai kwa ajili ya kuendesha na kukuza mchezo wetu katiaka mikoa yao.

TAVA inatoa rai kwa waalimu wote watakao nufaika na mradi huu, kuwa chachu ya maendeleo ya mchezo weto kwa kufanyia kazi kwa moyo, upendo na kwa kujitolea kuwafunza vijana wao mashuleni ili lengo letu lifikiwe. Vile vile kuwaomba wakuu wa mashule, Maafisa Elimu wa Mikoa, na wadau wote wa michezo kutoa ushirikianao wa hali ya juu katika kuwaruhusu na kuwawezesha waalimu kushiriki mafunzo hayo punde yanapofika katika mikoa yao. Aidha TAVA inashukuru Baraza la michezo la taifa kwa kuwezesha kupokea vifaa vyote vilipofika chini na kuvitunza hadi sasa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU