Mchezaji wa timu ya Twiga Stars Ester Chaburuma kulia akichuana na mchezaji wa Banyana Banyana Janne Van Wyk wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, katika mchezo huo Banyana Banyana imeshinda kwa goli 5-2 dhidi ya Twiga Star.
Magoli ya timu ya Banyana Banyana yamefungwa na wachezaji Portia Modise magoli mawili dakika ya 23 na 46, Sanah Mollo magoli mawili dakika za 73 na 79 Janine Van Wyk amefunga goli la tano dakika ya 86 ya mchezo huo
Magoli ya Twiga Stars yamefungwa na wachezaji Fatma Bashir dakika ya 63 kwa njia ya penati, huku goli la pili likifungwa na Asha Rashid dakika ya 77. Picha na full shangwe






0 maoni:
Post a Comment