Rais wa Cecafa Leodegar Tenga akizungumzia mashindano ya Kagame jijini Dar es Salaam (kulia) ni Katibu Mkuu wa Cecafa Nicolas Musonye
WAKATI pazia la mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama Kombe la Kagame Ikiratajiwa kufunguliwa rasmi Julai 14 na kufungwa Julai 29 Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Mshariki na Kati (Cecafa) imeshindwa kupata wadhamini wa mashindano hayo.
Kutoka na Cecafa kushindwa kupata wadhamini wa mashindano hayo timu zitakazo shiriki katika mwaka huu zitajitegemea wakati wa mashindano hayo.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais Cecafa Leodegar Tenga amesema hatua hiyo inatokana na kukosekana kwa wadhamini.
"Mpaka hivi sasa hatujapa wadhamini na hatuwezi kuacha kufanya mashindano kwani muda umekwisha na lazima yafanyike kuanzia katikati ya mwezi Julai mwaka huu"anasema Tenga na kuongeza:
"Ingawa bado tunaendelea kutafuta wadhamini timu zote zitakazo shiriki zinatakiwa zijiandae kugaramia usafiri wa kuwatoa katika nchi zao pamoja na garama za kukaa hapa nchini wakati huo sisi kama Cecafa tutajitahidi kuwasaidia katika suala la chakula,usafiri wa ndani pamoja na suala la waamuzi na makamisaa".
Tenga amesema kukuwa wadhamini wamekosekana mpaka hivi sasa amewaomba mashabiki watanzania na Afrika Mashariki kufika kwa wingi wakati wa mashindano ili kuzishangilia timu zao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Cecafa Nicolas Musonye amesema timu zote zitakazo shiriki katika mashindano hayo zitatakiwa kudhibitisha ushiriki wao mpaka Julai 25 na timu itakayoshindwa kufanya hivyo haita shiriki katika mashindano hayo.
0 maoni:
Post a Comment