Monday, June 4, 2012

VODACOM YAWAKUMBUS​HA WATEJA WA M PESA KUTUNZA NAMBA ZAO ZA SIRI

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzaniaimewatahadharisha wateja wao wa hudumaya M-pesa kuwa makini kulinda namba zaoza siri zisifahamike na watu wengine,kuepuka kuibiwa fedha zao.

Akizungunza na waandishi wa habari juzi ofisini kwakeMlimani city Jijini Dar es salaam, afisa mawasiliano na mahusiano JoselineKamuhanda ameelezea madhara yatokanayo na kuvuja kwa namba za siri za mteja,hali inayosababisha wizi.

“Ukweli mteja akitoa namba ya siri kwa wakala ili amsaidie kumtolea pesa katika akaunti yake nihatari, kwa vile itategemea wakala huyo atakuwa na uadilifu wa kiasi gani,lakini pia hata kwa mtu wa karibu kumpa kufahamu namba ya siri si jambo jema “ alisemaKamuhanda.

Akizungunzia kuboreshwa kwa mtandao huo alisema M-pesa imezidi kuimarika baada yakuondoa tatizo la ‘network’ kusumbua wakati Fulani, hali ambayo ililetamalalamiko kwa wateja.

“Tatizo la mtandao kusumbua katika zoezi utumaji pesa naupokeaji halipo baada ya wataalam kulifanyia kazi kikamilifu na kuliondoa”alisema Kamuhanda.

Akisisitiza kuhusiana na huduma za M-pesa afisa mkuu wabiashara Dylan Lennox amewaomba wateja kuwa na utamaduni wa kutuza namba zasiri ikibidi kuzibadilisha kila baada ya muda, kuzuia hata ndugu wa karibu aurafiki kuikariri namba hiyo.

“Kuna watu wapelelezi wa mambo anakuzoea inafikia kujuanamba ya siri ya akaunti yako, siku unataka kutioa fedha katikaakaunti yako unaambiwa huna fedha za kutosha, badala yake unalaumu Vodacomwamekuibia kitu ambacho si kweli” alisema Lennox.

Alisema tatizo la mteja kuibiwa linahusiana na yeye mwenyewekutoficha namba ya siri pengine kwa kutofahamu vyema namna ya njia za utoajifedha kwa njia ya M-pesa, bila kujua huyo aliyempa namba ya siri ameikalili na kutumia kumuibia.

Lennox anamalizia kwa kusema kuwa Voda com imejipanga vizuri zaidi kwa ajili ya kuwapa watanzania nawateja wote kwa ujumla kuwapa huduma bora za kisasa ili kujiendeleza katikamasuala ya kiuchumi na kijamii na kuwaomba watanzania waitumie vizuri hudumampya ya wajanja.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU