Saturday, June 30, 2012

WAHAMIAJI HARAMU WAZIKWA

 Baada ya kibali cha kuwazika nchini Tanzania wahamiaji toka Ethiopia waliofariki ndani ya lorry walilokuwa wanasafiria kutolewa na Serikali yao  ya Ethiopia, Serikali ya Tanzania iliamua mazishi ya Raia hao wa Ethiopia kufanyika Juni 29, 2012 Alasiri Mkoani Dodoma na Morogoro kwa baadhi ya miili iliyokuwa imehifadhiwa hospitali ya Mkoa Morogoro na kazi inayoendelea hapa ni ya uchimbaji wa makaburi.
 Vijana 84 wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakipita mmoja baada ya mwingine wakitoa heshima zao za mwisho na kuwaaga ndugu zao kwa kutupa udongo kwenye makaburi yaliyohifadhi miili ya wenzao waliopoteza maisha katika tukio la kusafirishwa kwenye Lorry.
 Kijana Chafamo Yosef (kulia) Muamiaji raia wa Ethiopia akitoa neno la shukrani muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazishi kwa jinsi ambavyo wamepatiwa msaada na serikali ya Tanzania tangu siku walipokutwa wametelekezwa, miongoni mwa vitu alivyoahidi akifika nchini kwao Ethiopia ni kuwaelezea watu wa Ethiopia kuwa walidanganywa na kusababishiwa matatizo makubwa hadi baadhi yao kupoteza maisha lakini wao Mungu amewanusuru, wameona nchi nzuri ya Tanzania, wamekutana na serikali nzuri iliyowahudumia kila kitu, na wananchi wenye mioyo ya huruma na ukarimu.
 Raia wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kuwaombea sala wenzao waliopoteza maisha wakati wa shughuli ya mazishi.
 Safari ya mwisho ya kuwasindikiza na kuwahifadhi katika nyumba zao za milele wahamiaji 43 (21 Dodoma, 23 Morogoro) kutoka Ethiopia waliopoteza Maisha ilihitimishwa kwa kazi ya kufukia makaburi iliyofanywa na vijana na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye mazishi hayo.
 Wahamiaji hawa (walionusurika) wamekuwa watu waliozamia katika sala na maombi baada ya kunusurika kifo ukizingatia baadhi ya wenzao walikufa katika tukio hilo, kila baada ya chakula jioni wanapewa muda wa kufanya maombi.
 Wahamiaji kutoka Ethiopia walipatiwa kila aina ya msaada wa muhimu uliohitajika kwa wakati kama malazi, mavazi, chakula dawa,  matibabu ya kisaikolojia nk
 Mtoa huduma ya kwanza wa Msalaba Mwekundu akimfunika mmoja wa wahamiaji kutoka Ethiopia ambaye alikuwa na tatizo la maumivu kifuani.
 Vijana walioandaliwa kwa ajili ya shughuli ya Mazishi wakishusha miili ya Marehemu kwenye nyumba zao za milele (makaburi) ikiwa ni hatua za mwisho za kuhitimisha safari ya mwisho ya kuwapumzisha watu hao waliopoteza maisha.
 Vijana Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakilia kwa uchungu muda mfupi baada ya miili ya Wenzao waliopoteza maisha kuwasili eneo la maziko mjini Dodoma, jumla ya Waethiopia 43 walipoteza maisha ambapo 21 wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro.
Vijana Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wamejipanga mistari miwili wakionekana wenye huzuni muda mfupi baada ya kuwasili eneo lililoandaliwa katika Manispaa ya Dodoma kwa ajili ya kuwazika wenzao waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, jumla ya Waethiopia 43 walipoteza maisha ambapo 21 wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro. Picha zote na Jery Mwakyoma

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU