Wednesday, July 18, 2012

UN NA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI WAADHIMISHA MIAKA 94 YA NELSON MANDELA KWA KUIKARABATI SHULE YA MSINGI TANDALE.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini wakiwa wamekusanyika katika shule ya Msingi Tandale jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyakazi za kujitolea kwa dakika 67 ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 mwezi Julai.
Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mh. Ibrahim Mukiibi akiwasili kushiriki zoezi hilo.
Mabalozi wa Afrika Kusini Mh. Henry Chiliza (kushoto) na Mh. Ibrahim Mukiibi wa Uganda wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wakisalimiana baada ya kukutana katika zoezi la kujitolea kufanya kazi za kijamii katika shule ya msingi Tandale ya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joymrey Von de Merwe.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitoa mwongozo wa namna ya kutekeleza zoezi hilo ambalo limeonyesha mafanikio makubwa baada ya kuweza kukarabati madawati yalioharibika, kupiga rangi Ubao za kuandikia madarasani na kufanya usafi katika mazingira ya shule hiyo.
Bi. Stella Vuzo amesema katika kuadhimisha siku kama hii mwaka jana Umoja wa Mataifa ulitoa huduma za Kibinadamu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Saratani na mwaka huu wameonelea ni vyema kuungana na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale kwa kuonyesha wanajali na kutoa huduma kama hizo katika shule hiyo chini ya kauli mbiu ya mzee Nelson Mandela "Inspire Change Within Your Self".
Wafanyakazi wa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini wakishirikiana kubeba madawati kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati.
Pichani Juu na Chini ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Tandale jijini Dar Hamisi Kubiga (kushoto) sambamba na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mh. Henry Chiliza wakihakikisha ukarabati wa madawati unakwenda sawa.
Balozi wa Uganda nchini Mh. Ibrahim Mukiibi akifanya usafi katika moja ya madarasa ya Shule hiyo.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitumia muda wake wa dakika 67 kusafisha maeneo ya shule ya msingi Tandale ya jijini Dar.
Mfanyakazi wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Masoud Ramadhani (kushoto) akichanganya dawa kwa ajili ya kusafisha vyoo vya shule ya msingi Tandale katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Wanafunzi na wafanyakazi wa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini wakisaidiana kuzoa taka kuhakikisha shule ya msingi Tandale inakuwa safi.
Wanafunzi wakionyesha ushirikiano katika kuadhimisha Nelson Mandela International Day.
Pichani Juu na Chini Wafanyakazi wa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini wakipiga rangi Ubao wa Kufundishia katika shule ya msingi Tandale jijini Dar es Salaam.

Afisa Mawasiliano wa UNICEF Jacquiline Namfua (kushoto) na wafanyakazi wenzake wakishiriki kupiga rangi katika moja ya ubao wa shule hiyo kuhakikisha wanafunzi wanapata mahali sahihi pakufundishiwa.
Mmoja wa watu aliyejitolea Kapteni wa Ndege Bw. Andre Van Devententer akishirikiana na wanafunzi wa shule ya msingi Tandale kukarabati madawati mabovu katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela leo.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Bi. Stella Vuzo akiwa katika moja ya darasa na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ambao mpaka leo wana uhaba wa madawati hivyo kulazimika kukaa chini wakati wa kusoma.
Wanafunzi wa shule ya msingi Tandale wakibanana katika dawati moja mithili ya abiria ndani ya Dalala huku tukitegemea kuboreka kwa kiwango cha elimu nchini.
Masoud Ramadhani wa Ubalozi wa Afrika Kusini akiosha moja ya Vyoo vya shule hiyo.
Balozi wa Afrika Kusini nchini Mh. Henry Chiliza akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika shule ya Msingi ya Tandale ambapo amesisitiza siku hii ya Kimataifa ya Mandela inaadhimishwa kwa kufanya shughuli za kijamii kwa kuwa Mzee Mandela mwenyewe alikuwa akijitolea muda wake mwingi kusaidia watoto, kufanya shughuli za kijamii, kutetea haki za watoto na wanyonge.
Pichani Juu na Chini Balozi wa Afrika Kusini nchini Mh. Henry Chiliza akikabidhi msaada wa uliotolewa na UN kwa Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo Lucy Mwakibete huku wakishuhudiwa na wafanyakazi wa UN, Ubalozi, Walimu na wanafunzi.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tandale Bi. Lucy Mwakibete (katikati) akitoa shukrani kwa UN na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini ambapo ameelezea changamoto mbalimbali zinazoikabili shule zikiwemo Uhaba wa Madawati, Vyoo, Ubovu wa Sakafu za Vyumba vya Madarasa na kuwaomba wadau kujitokeza kuwasaidia ili kuboresha mazingira mazuri kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Kutoka kushoto ni Kansela wa Masuala ya Siasa Bw. Terry Govender na Joymery Von De Merwe kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Tandale Bi. Lucy Mwakibete.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU