Warembo wa Redds Miss Sinza wakiwa mazoezini kwenye ukumbi wa Mawela social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican chini ya mwalimu wa, Mwajabu Juma ambaye anashikiria taji la Top Model . Warembo hao watapanda jukwaani Julai 13 kutafuta tiketi ya kuiwakilisha Sinza katika mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
JUMLA ya warembo 15 wamejitokeza kuwania taji la Mrembo wa Sinza “Redds Miss Sinza 2012” yaliyopangwa kufanyika julai 13 kwenye ukumbi wa Mawela social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hotel ya Vatican City.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary wa kampuni ya Calapy Entertainment aliwataja warembo hao kuwa ni Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva Mushi, Vailet John, Esther Mussa, Christina Samwel, Nahma Said, Shadya Ali, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Majuto alisema kuwa warembo hao wapo kambini chini ya mwalimu wao, Mwajabu Juma ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss Tanzania Top Model. Alisema kuwa mazoezi ya warembo hao yanafanyika kwenye ukumbi wa mashindano hayo, Mawela social kuanzia saa 8.30 mchana.
“Warembo wamepania kufanya kitu cha kihistoria siku ya mashindano nah ii inatokana na ukweli kuwa wamejiandaa vilivyo na kwa sasa wanamalizia tu baadhi ya vitu vidogo vidogo vya mashindano hayo, alisema Majuto.
Alisema kuwa lengo kubwa la mashindano ya mwaka huu ni kutwaa taji la Redds Miss Tanzania mbali ya taji la Kanda ya Kinondoni katika shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.
“Tuna warembo moto wa kuotea mbali ambao kwa sasa wameonyesha kupania kufanya kile ambacho kimesubiliwa na wadau wa warembo wa mitaa ya Sinza na vitongoji vyake, hii inatokana na ukweli kuwa mashindano haya ni ya mwisho kwa upande wa vitongoji jijini,” alisema.
0 maoni:
Post a Comment