Meneja wa banda la Windhoek Jerome Rugemalila akiokota moja ya kuponi kwenye boksi la Bahati nasibu ya Airtel wakati Airtel ilipochezesha Bahati nasibu jana kwa wateja wake wanaonunua bidhaa mbalimbali katika maonyesho ya 36 ya biashara kwenye viwanja vya Sabasaba Temeke.
Airtel ilivyojipanga na zawadi kwaajili ya wateja wake wanaonunua bidhaa mbali mbali na kulipia kwa njia ya Airtel money. ukinunua bidhaa katikakijiji cha Airtel, banda la Windhoek, hupata kuponi ambazo baadae huzungushwa na huibuka washindi wa kati ya zawadi hizo zikiwemo simu za mkononi aina ya sumsung, Modem yenye kasi ya 3.75G pamoja na shilingi 2,000 kwa jumla ya wateja 60 kwa siku
Kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Tanzania akifuatilia watoa huduma wa banda la Windhoek wanavyoelekezena jinsi ya kununua bidhaa katika banda lao kwa kutumia huduma ya Airtel Money
MC na mtangazaji wa ofa katika banda la Windhoek akitangaza namba ya mshindi wa simu katika kuponi wakati wa Bahati nasibu ya Airtel ilipochezeshwa jana maalum kwa wateja wake wanaonunua bidhaa mbalimbali katika maonyesho ya 36 ya biashara kwenye viwanja vya Sabasaba Temeke.
0 maoni:
Post a Comment