Tuesday, July 17, 2012

YANGA YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA EL-SALAM WAU KWA MABAO 7-1

 Kiungo wa Yanga,Nizar Khalfan akichuana na Beki wa El- Salam Wau wakati wa mchezo wao wa Mashindano ya Kagame.

 Yana ya jijini Dar es Salaam, leo imeibuka na ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya timu yaEl-salam Wau ya Sudan Kusini, mechi iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Mabao ya Yanga yalifingwa na Hamis Kiiza mabao matatu, Said Bahanuzi mabao mawili, Stefano Mwasyika na Nizar Khalfan kila mmoja bao moja.

Sudan Kusini, bao lao lilifungwa dakika ya 88, kupitia kwa Hamis Bashama.Katika mechi ya kwanza iliyopigwa uwanjani hapo kati ya APR ya Rwanda na Atletico ya Burundi, timu hizo zilitoka suluhu.

Kwa matokeo hayo, APR,Atletico na Yanga zimetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, Huku El-Salam Wau inayoshiriki kwa mara ya kwanza ikisubiri mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Atletico, Yanga wao watakua na kibarua kigumu dhidi ya APR.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU