Monday, July 16, 2012

YUSSUF MANJI NDIE MWENYEKITI MPYA WA YANGA

Mwenyekiti mpya wa yanga Yussuf Manji na Makamu wake Clement Sanga


Kutokana na uchaguzi mdogo wa Viongozi wa Clabu ya Yanga uliofanyika jana Julai 15,2012 Mfadhili mkubwa wa Klabu ya Yanga, Yussuf Manji, ndie ameibuka Mshindi kwa nafasi ya Mwenyekiti, na Makamu mwenyekiti ni Clement Sanga. Huku Nafasi za wajumbe zikishikiliwa na Abdallah Bin Klebu, Aron Nyanda, Mussa Katabaro na George Manyama  katika Uchaguzi mdogo wa Klabu hiyo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall Jijini Dar es Salaam.
Zoezi la kuhesabu kura za Uchaguzi huo wa kuziba nafasi za wazi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji liliendelea hadi Usiku wa manane.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU