Monday, July 2, 2012

KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATUPILIA MBALI PINGAMIZI ALILOWEKEWA YUSUPH MANJI


Yusuf Manji

Kamati ya uchaguzi ya TFF ilikutana Jumapili ya Julai 01,2012 na Jumatatu ya Julai 02,2012 kupitia mchakato mzima wa uchunguzi wa kuziba nafasi zilizo wazi kwenye uongozi wa klabu ya Yanga na pia kusikiliza rufaa ya Ishabakari Luta dhidi ya maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuhusu maombi ya mwombaji uongozi wa Yanga Ndugu Yusuf Manji kugombea nafasi ya Mwenyekiti.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia rufaaa hiyo na kufikia maamuzi yafuatayo:-
1. Kwa kuwa mrufani hakutimiza matakwa ya kanuni za uchaguzi ibara ya 11 (2) ambayo inataka mrufani kuweka vielelezo vya rufaa yake, anuani ya kudumu na saini yake:

2. Kwa kuwa mrufani hakutokea kutetea rufaa yake, 

Kamati ya Uchaguzi TFF imetupilia mbali rufaa ya Ishabakaki Luta.

1 maoni:

Anonymous said...

hivi pingamizi haliwezi kujadiliwa bila kuwepo kwa aliyeliweka?kuna mazingira gani ya usalama wa mweka pingamizi?mimim nafikiri cha msingi ni hoja zilizoko kwenye pingamizi,kama zitamhitaji mweka pingamizi au vielelezo ndipo zitupwe au kukubaliwa,sio watu wakae kikao,walipwe posho halafu wasijadili pingamizi,lazima kuwe na value for money

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU