Monday, September 24, 2012

BIA YA BALIMI EXTRA LAGER YAZINDUA UTAMBULISHO MPYA WA KANDA YA ZIWA.

 Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Eng.Francis Mnkabenge (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya  uzinduzi wa chupa kubwa ya bia ya balimi ambayo ni maalum kwa watu wa kanda ya ziwa itakayopamba mandhari ya jiji la Mwanza iliyowekwa katikati ya jiji barabara ya Pamba kulia ni Meneja wa Meneja wa bia hiyo Edith Bebwa,  na Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Malaki Siraki.
 Meneja wa bia maalum kwaajili ya watu wa kanda ya ziwa ya Balimi, Edith Bebwa, (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Eng.Francis Mnkabenge (katikati) na Meneja wa Mauzo na Usambazaji wa TBL Malaki Siraki wakishuhudia uzinduzi wa chupa kubwa ya bia hiyo itakayopamba mandhari ya jiji la Mwanza iliyowekwa katikati ya jiji barabara ya Pamba.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua utambulisho mpya wa kanda ya Ziwa.
 
Bia inayoongoza kwa mauzo katika kanda ya ziwa na iliyobeba jina lenye asili ya mikoa ya kanda hiyo “Balimi Extra Lager” leo imefanya uzinduzi wa aina yake wa alama mpya itakayotambulisha kanda ya ziwa ikiwa ni pamoja na alama nyingine zilizokuwepo tangu awali. Alama hii ambayo ni chupa kubwa na ya aina yake ya Bia ya Balimi imesimikwa katika mnara mrefu katika makutano ya barabara za Pamba na Miti Mirefu na kuifanya ionekane tokea umbali mrefu wa zaidi ya mita 500.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa Bia ya Balimi Bi. Edith Bebwa alisema, Bia ya Balimi Extra Lager ilianzishwa rasmi mwaka 1999 ikiwa ni tuzo maalum kwa wakazi wa kanda ya Ziwa kwa kazi nzuri wanazofanya katika sekta za Kilimo, uvuvi, madini nk. Tangu mwaka huo, bia hii imekuwa ikipendwa sana na hata kuwa bia inayoongoza kwa mauzo kuliko bia zote kwa kanda ya Ziwa. Kitu kikubwa kinachoipa bia ya Balimi mafanikio haya ni ladha yake ya kuvutia na ubora wa hali ya juu wa bia hii. Zaidi ya yote hayo ni jina la bia hii ambalo lilitolewa kwa heshima kubwa ya kanda ya ziwa “BALIMI” likimaanisha “WAKULIMA”. Kuna mambo mengi ambayo hutumika kuitambulisha kanda yetu ya ziwa, ikiwa ni pamoja mawe maarufu yaliyobebana “Bismark Rocks”. Hivyo leo tunayofuraha kubwa kuzindua alama mpya itakayoongeza vitambulisha vya kanda yetu, nayo ni chupa kubwa,nzuri na ya kuvutia ya “BALIMI EXTRA LAGER” kipenzi cha kanda ya ziwa. Alisema Edith.
 
Nae meneja wa Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa Bw. Malaki Sitaki alielezea mchango mkubwa ambao bia ya Balimi inatoa katika kanda ya ziwa kwa kuainisha maeneo mbalimbali ya udhamini akisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa karibu sana na wakazi wa kanda ya Ziwa kwa kuhakikisha inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza michezo na tamaduni za kanda yetu ya ziwa. Bia hii inadhamini mashindano maarufu ya Mitumbwi yanayofanyika kila mwaka kanda ya Ziwa. Pia inadhamini mashindano ya ngoma za asili za kanda ya ziwa na vile vile inadhamini tamasha la kudumisha utamaduni wa mkoa wa Tabora lijulikanalo kama “Tamasha la Mtemi Mirambo. Haya ni baadhi tu ya mambo mengi ambayo bia ya Balimi inafanya, hivyo tunaomba wakazi wa kanda ya ziwa waendelee kuiunga mkono bia hii ili iweze kuwafanyia mambo makubwa zaidi, maana wahenga walisema “Jivunie Kilicho Chako. Hii ni kanda yetu, na Balimi extra Lager ni Bia yetu”. Alimaliza Bw. Malaki

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU