BINGWA wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC,
Francis Cheka 'SMG' usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kwamba hana mpinzani
katika ngumi hizo nchini baada ya kumchapa kwa KO mpinzani wake mkubwa, Karama
Nyilawila na kuongeza taji jingine.
Cheka alimpiga Nyilawila katika
raundi ya sita ya pam,bano hilo lililokuwa la uzani wa Super
BINGWA wa ngumi za kulipwa
anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC, Francis Cheka 'SMG' usiku wa
kuamkia leo amedhihirisha kwamba hana mpinzani katika ngumi hizo nchini baada ya
kumchapa kwa KO mpinzani wake mkubwa, Karama Nyilawila na kuongeza taji
jingine.
Cheka alimpiga Nyilawila katika
raundi ya sita ya pam,bano hilo lililokuwa la uzani wa Super Middle la raundi 12
lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar es Salaam na kutwaa
ubingwa wa Mabara wa UBO uliokuwa wazi.
Pambano hilo lililohudhuriwa na
mashabiki lukuki, lilishuhudia raundi zote tano za kwanza Nyilawila akionyesha
kumdhibiti Cheka kwa kumchezea 'kibabe' akitumia nguvu nyingi kujihami na baadhi
ya watu ukumbini kuamini mwisho wa tambo za Cheka zilikuwa zimewadia.
Hata hivyo raudni ya sita ilipoanza
Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha wake Abdallahj Saleh
'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo
Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani
wake.
Mwamuzi wa pambano hilo, Jerome
Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka, lakini ghafla
akaonyesha ishara kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo na ukumbi mzima
kuripuka kwa shangwe akishangiliwa Cheka ambaye hiyo ni mara ya pili kumpiga
Nyilawila.
Kabla ya pambano hilo lililoanza
majira ya saa 3;40 usiku, kulikuwa na mapambano saba ya utangulizi pamoja na
burudani ya muziki toka bendi ya Mashujaa ambao hata hivyo sio wapenzi wengi
walioweza kuishuhudia kutokana na kuondoka ukumbini mapema.
Katika pambano la kwanza la
utangulizi Said Mbelwa alimpiga kwa pointi Dickson Mwakipesile, Juma Kihiyo
alipigwa kwa pointi na Ibrahim Mahokola katika pambano lililovutia kwa namna
mabondia hao walivyoonyeshana kazi.
Pia mdogo wa Cheka, Cosmas Cheka
alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Fadhil Awadh katika pamnbano
jingine lililosisimua wengi kwa ufundi uliokuwa ukionyesha na mabondia hao, naye
Shaaban Kilumbelumbe alimpiga kwa pointi Anthony Mathias kabla ya Safari Mbiyu
kumpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Khalfan Jumanne.
Michezo minginme iliwakutanisha Stan
Kessy na Seba Temba, pambano lililoisha kwa mabondia hao kutoka sare na Hassani
Kidebe alitolewa nishai na Deo Samwel kwa kupigwa kwa pointi.
Mgeni rasmi katika pambano hilo
alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ambaye aliutangazia umma
kwamba kama Mlezi wa Ngumi za Kulipwa amefanikiwa kuwafuta wafadhili katika
mchezo huo na kumtambulisha raia mmoja wa kigeni kwamba ni miongoni
mwao.
Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Temeke jijini
Dar es Salaam na kutwaa ubingwa wa Mabara wa UBO uliokuwa wazi.
Pambano hilo lililohudhuriwa na
mashabiki lukuki, lilishuhudia raundi zote tano za kwanza Nyilawila akionyesha
kumdhibiti Cheka kwa kumchezea 'kibabe' akitumia nguvu nyingi kujihami na baadhi
ya watu ukumbini kuamini mwisho wa tambo za Cheka zilikuwa zimewadia.
Hata hivyo raudni ya sita ilipoanza
Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha wake Abdallahj Saleh
'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo
Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani
wake.
Mwamuzi wa pambano hilo, Jerome
Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka, lakini ghafla
akaonyesha ishara kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo na ukumbi mzima
kuripuka kwa shangwe akishangiliwa Cheka ambaye hiyo ni mara ya pili kumpiga
Nyilawila.
Kabla ya pambano hilo lililoanza
majira ya saa 3;40 usiku, kulikuwa na mapambano saba ya utangulizi pamoja na
burudani ya muziki toka bendi ya Mashujaa ambao hata hivyo sio wapenzi wengi
walioweza kuishuhudia kutokana na kuondoka ukumbini mapema.
Katika pambano la kwanza la
utangulizi Said Mbelwa alimpiga kwa pointi Dickson Mwakipesile, Juma Kihiyo
alipigwa kwa pointi na Ibrahim Mahokola katika pambano lililovutia kwa namna
mabondia hao walivyoonyeshana kazi.
Pia mdogo wa Cheka, Cosmas Cheka
alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Fadhil Awadh katika pamnbano
jingine lililosisimua wengi kwa ufundi uliokuwa ukionyesha na mabondia hao, naye
Shaaban Kilumbelumbe alimpiga kwa pointi Anthony Mathias kabla ya Safari Mbiyu
kumpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Khalfan Jumanne.
Michezo minginme iliwakutanisha Stan
Kessy na Seba Temba, pambano lililoisha kwa mabondia hao kutoka sare na Hassani
Kidebe alitolewa nishai na Deo Samwel kwa kupigwa kwa pointi.
Mgeni rasmi katika pambano hilo
alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ambaye aliutangazia umma
kwamba kama Mlezi wa Ngumi za Kulipwa amefanikiwa kuwafuta wafadhili katika
mchezo huo na kumtambulisha raia mmoja wa kigeni kwamba ni miongoni mwao.
0 maoni:
Post a Comment