YANGA SC imepata ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Hadi
mapumziko Yanga walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na
Nahodha, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya nne na Didier Kavumbangu
dakika ya 31, mabao yote yakitokana na kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji Simon
Msuva.
Bao la
kwanza ulikuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima, baada ya Msuva
kuangushwa karibu kabisa na eneo la hatari la JKT Ruvu na bao la pili dogo huyo
aliyesajiliwa kutoka Moro United iliyoshuka daraja, alimpa pasi mshambuliaji wa
kimataifa wa Burundi, Kavumbangu.
Kipindi cha
pili, Yanga walirudi tena kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya
52, mfungaji Simon Msuva kabla ya Didier Kavumbangu kufunga la nne dakika ya 65.
JKT ilipata
bao lake la kufutia machozi dakika ya 68 mfungaji Credo Mwaipopo. Picha na Bin Zubeiry
0 maoni:
Post a Comment