Mkurungezi
wa spanco Tanzania bw Chandrashekhar Narayanan akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo
Airtel imesherehekea na wateja wake kwa kuwashukuru kwa kutumia huduma
Zake, Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel bi
Adrianna Lyamba na kulia ni Meneja uendeshaji Amit Arora.
Spanco
Country Head for Tanzania Mr. Chandrasekhar Narayanan speaks to the
press on customer service week were Airtel celebrates by thanking its
customer for choosing Airtel as preferred network service provider. On
the left is Airtel Customer Care Director Adrianna Lyamba and on the
right is Spanco Operation Manager Amit Arora
Mkurugenzi
wa Airtel Sam Elangallor akiongea na waandishi wa habari wakati wa
maathimisho ya wiki ya ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo Airtel
imesherehekea na wateja wake kwa kuwashukuru kwa kutumia huduma Zake Airtel
Managing Director Sam Elangallor speaks to the press on customer
service week were Airtel celebrates by thanking its customer for
choosing Airtel as preferred network service provider.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya
huduma kwa mteja duniani kwa kutoa na kuahidi kuendelea kutoa huduma
bora na za kisasa kwa wateja wake hapa nchini.
Ahadi
hiyo imetolewa na Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Bw. Sam
Elangalloor leo Jijini dar ikiwa ni katikati ya maadhimisho ya wiki ya
huduma kwa wateja wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania bw Sam Elangalloor alisema “Airtel
imejipanga kutoa huduma bora na za kimataifa kwa kuwa tumewekeza
kikamilifu katika vitendea kazi vya kisasa na pia tunashirikiana
kikamilifu na wadau wetu wataalam wa huduma kwa wateja SPANCO RAPS
–Tanzania Limited ili kumpatia mteja huduma yenye ubora zaidi kila
wakati, tunawatoa huduma zaidi ya 650 wakitoa huduma masaa 24 siku 7 za
wiki. Airtel tutaendelea na dhamira yetu hii ya kutoa huduma bora na ya
kisasa ili kuendelea kuvutia wateja wengi kutumia mtandao wa Airtel
pamoja na kutimiza malengo yao mbalimbali.”
Sam
aliendelea kwa kusema” tumewekeza kwa kiasi kikubwa kupanua wigo wa
mawasiliano hasa vijijini na hivyo tumekuwa na ongezeko kubwa la wateja
wanaojiunga kwenye huduma zetu. Leo asilimia 97 za simu zinazopigwa
kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja ni zakutaka ufafanuzi wa namna
ya kutumia huduma zetu za Internet, meseji, namna ya kutumia simu,
Airtel money na nyingine zinazofanana na hizo.
Vileviele
Airtel tumewekeza kikamilifu katika mfumo wetu wa ndani na nje wa
mawasiliano kwa kuweka miundombinu ya kisasa kwa lengo la kuwahudumia
wateja kwa haraka na urahisi zaidi. Airtel tunaushirikiano mkubwa na IBM
wataalam wakubwa katika teknolojia ya mwasiliano duniani ikiwa ni
muendelezo wa kutimiza dhamira yetu kuhakikisha tunatoa mawasiliano
bora na nafuu kwa kumfaidisha mteja wetu wakati wote atumiapo huduma za
Airtel” aliongeza bw Elangalloor.
Kwa
upande wake mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba
alisema” tunao wafanyakazi waliopata mafunzo na wanaoendelea kupewa
mafunzo mbalimbali ili kwenda na mabadiliko mbalimbali ya technologia za
kisasa. Hivi karibuni tulizindua Mafunzo ya muda mrefu yajulikanayo
kama Airtel Service Academy ili kuwawezesha wafanyakazi wetu kuongeza
ufanisi kwa kupitia mafunzo haya”.
Sambamba
na hilo tumewekeza kwenye technolojia za kisasa ili kuwawezesha wateja
wetu kutufikia kirahisi kupitia call center zetu. Leo tunayofuraha
kuweza kuwasiliana na wateja wetu nchi nzima kupitia mawakala au kwa
kupiga namba 0784001001
bila malipo na kuweza kupata taarifa mbalimbali zikiwemo ofa kabambe,
huduma za internet, kupiga na kutuma ujumbe mfupi na nyingine nyingi”
Airtel
call center inapatikana masaa 24 siku 7 za wiki, na tunapokea simu
zaidi ya laki moja kwa siku hii ni kutokana na wateja wetu wengi kutumia
huduma za simu na internet mara ya kwanza,
Maduka
yetu yanafunguliwa kuanzia saa 2 hadi saa moja usiku, ili kuweza mteja
wetu ili kuwasiliana nasi tafadhali piga namba 100 bure au piga +255 78 4105 400, +255 78 4104 800 ikiwa unatumia
namba ya mtando mwengine na utatozwa gharama ya kupiga simu ya
kawaida, vilevile unaweza kutupata kwa kupitia barua pepe Email info@tz.airtel.com.” aliongeza Lyamba.
Nae
Mkurugenzi wa Spanco Tanzania Chandrashekhar Narayanan alisema”
tunayofuraha kushirikiana na Airtel katika kutoa huduma bora kwa wateja
Tanzania. Tunaamini huduma bora tunayoitoa inafanikisha lengo la Airtel
la kuwa mtandao unaopendwa na watanzania nchini. Tunauzoefu wa kutoa
huduma kwa wateja katika nchi mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na
kupokea simu za wateja zaidi ya 400000 kwa siku”
Wiki
ya huduma kwa wateja huadhimishwa tarehe mosi hadi tano ya mwezi October
Duniani kote na hapa nchini kampuni ya Airtel yenye wateja zaidi ya
milioni 8 inafanya maadhimisho hayo kwa shughuli mbalimbali huku kauli
mbiu yao ikiwa ni “ Ni mimi wa kukupa huduma bora “ Airtel inadhihirisha mteja ni muhimu
Airtel
ni mtandao wenye gharama nafuu na wenye mtandao mpana ulioenea zaidi
kwa utoa huduma kama vile Airtel money ambayo imewezesha upatikanaji wa
huduma za kifedha kirahisa kwa gharama mahali popote nchini.
0 maoni:
Post a Comment