Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko
wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam
katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya
wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre,leo Oktoba 26, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa waumini wa Kiislam wa Kijiji cha Vuchama wakati akiondoka eneo hilo baada ya kuzindua na kuweka Jiwe la Msingi na kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. leo Oktoba 26, 2012.
0 maoni:
Post a Comment