Katibu Tawala Wilaya ya Moshi Mjini ,
Hashimu Shimbo(kulia) akiwakabidhi Kikombe wachezaji wa klabu ya Polisi
Baalax mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya
Darts Taifa(TADA) yaliyofanyika katika Hoteli ya Hugo’s Moshi Mkoani
Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
POLISI Balax ya
jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika mashindano ya Taifa ya
Darts (TADA) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mjini Moshi, Mkoani
Kilimanjaro na kujitwalia Kikombe na pesa taslimu shilingi laki
tatu(300,000/=) pamoja na cheti cha ushiriki.
Polisi Balax waliupata Ubingwa huo kwa kichapa timu ya Friends
ya jijini Daar es Saalaam 9-2 hivyo kufanikiwa kupata nafasi ya kwanza
ambapo nafasi ya pili ilikamatwa na Friends ambao walizawadiwa pesa
taslimu shilingi laki mbili na cheti cha ushiriki,nafasi ya tatu
ilichukuliwa na VIP ya Arusha ambayo ilizawadiwa shilingi laki moja na
cheti cha ushiriki.
Katika
Singles(mchezaji mmoja mmoja) wanaume nafasi ya kwanza ilichukuliwa na
Wambura Msira kutoka klabu ya Lugalo ya jijini Dar es Salaam ambaye
alijinyakulia pesa taslimu shilingi laki mbili na cheti cha ushiriki
ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Syliwa Revocatus kutoka klabu ya
VIP Arusha ambaye alijinyakulia pesa taslimu shilingi laki moja na nusu
na cheti cha ushiriki.
Kwa upande wa Wanawake Singles mshindi wa kwanza alichukua Irene Kiluki kutoka Klabu ya Kimanga
ambaye alijinyakulia pesa taslimu shilingi laki moja na nusu pamoja na
cheti cha ushiriki ambapo mshindi wa pili alichukua Vicky Mdiki kutoka
Klabu ya Moshi na kujinyakulia pesa taslimu shilingi laki moja na cheti
cha ushiriki
Fainali
za mashindano hayo zilihudhuriwa na mgeni rasmi,Katibu Tawala Wilaya ya
Moshi Mjini , Hashimu Shimbo ambaye aliwashukuru viongozi na wachezaji
kwa kufanya mashindano hayo ya Kitaifa katika mji wa Moshi Mkoa wa
Kilimanjaro unaonngoza kwa usafi Tanzania,pia aliipongeza Kampuni ya Bia
Tanzania kwa kudhamini mchezo wa Darts na kuwaomba wasichoke kudhamini
na kuendeleza mchezo huo nchini kote
Shimbo
alisema Serikali iko tayari kushirikiana na wadhamini
,wadau,vilabu,Wilaya na Mikoa kurudisha mchezo wa Darts kwenye thamani
yake ya zamani.
0 maoni:
Post a Comment