Monday, October 22, 2012

WANAFUNZI BUGURUNI VIZIWI NA BALOZI WA AIRTEL AY-WAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA VIFAA VYA KUFUNDISHIA

Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea na wanafunzi wa shule ya Buguruni Viziwi mwishoni mwa wiki hii wakati ambapo airtel walitembelea shule ya msingi viziwi kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia pamoja na nyenzo mbalimbali kupitia mradi maalumu wa kuchangia vitabu unaoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA, kushoto ni Mwalimu wa shule hiyo bi Judith Kaneno akifuatiwa na Airtel Ambassador ajulikanae kwa jina la AY( Ambwene Yessaya) kulia ni Mwalimu mkuu bi. Winfrid Jeromia.
 Mwalimu wa shule ya msingi Buguruni Viziwi akiwapa ujumbe wanafunzi wa shule hiyo baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Airtel, kutoka kushoto ni mwamlimu mkuu wa shule hiyo bi Winfrid Jeromia, akifuatiwa na Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi na Airtel Ambassador Ambwene Yessaya (AY). Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia
 Meneja huduma za jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiangalia ujuzi wa wanafunzi wa shule ya Buguruni viziwa alipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii. wakati AIRTEL na Balozi wao msanii AY walipofanya ziara maalum ya kuhamasisha jamii kuchangia wanafunzi hao wa shule ya msingi Buguruni viziwi kupata vifaa vya kujifunzia kwa kushirikiana na BAMVITA
Balozi wa Airtel  nchini Ambwene Yessaya (AY) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chekechea ya shule ya msingi Buguruni Viziwi walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii.Airtel kwa kushirikiana na BAMVITA wanaendesha mradi maalum utakaowezesha wanafunzi hao wenye uhitaji maalum kupata vifaa vya kujifunzia

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU