Saturday, October 6, 2012

YANGA, AFRICAN LYON KUTOVAA BEJI YA MDHAMINI

Kwa vile msimu huu mdhamini mwenyewe ndiye anayegawa vifaa kwa timu, Kamati ya Ligi imeagiza Vodacom iandikiwe barua na nakala kwa klabu zote ili kujua timu ambazo tayari zimekabidhiwa vifaa hivyo zikiwemo logo na siku ambapo timu husika zilipokea.
 
Baada ya majibu ya Vodacom ndipo Kanuni za Ligi Kuu zitakapotumika kutoka adhabu kwa timu ambazo zitabainika kuwa zilipokea vifaa lakini hazikuvitumia.

MECHI YA KAGERA SUGAR, YANGA YASOGEZWA
Kamati ya Ligi imesogeza mbele kwa siku moja mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar na Yanga iliyokuwa ichezwe kesho (Oktoba 7 mwaka huu) mjini Bukoba kutokana na Uwanja wa Kaitaba kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
 
Sasa mechi hiyo itachezwa Jumatatu (Oktoba 8 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo. Mabadiliko hayo pia yameathiri mechi kati ya Toto Africans na Yanga iliyokuwa ichezwe Oktoba 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 11 mwaka huu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU