Monday, November 26, 2012

AIRTEL YAGAWA VITABU VYA MILIONI 16 DAR

 Mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vitabu kwa shule za sekondari, kaimu afisa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya akizungumza machache kabla ya kukabidhi vitabu kwa shule zipatazo 8 kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanayo kama ' AIRTEL SHULE YETU'.
 Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kiduma Mgeni akitoa nasaha zake kwa walimu na wanafunzi waliohudhuria katika hafla hiyo.
 Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi (Kulia) akimkabidhi vitabu mgeni rasmi, kaimu afisa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kwanza kushoto) kwa niaba ya shule za sekondari zipatazo 8 kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ujulikanao kama ' AIRTEL SHULE YETU'. Walioshuhudia ni maofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kulia) akiwakabidhi vitabu Maofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kiduma Mgeni (Kushoto) na mwenzake kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanayo kama ' AIRTEL SHULE YETU'.
 Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kulia) akiwakabidhi vitabu wanafunzi wa shule ya sekondari ya Yemeni ambao walipokea kwa niaba ya wanafunzi wenzao. Pembeni anayeshuhudia ni Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi.
 Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Yemeni wakifurahia vitabu mara baada ya kukabidhiwa na Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi.
 Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kulia) akimkabidhi vitabu mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Yemeni mwalimu Antipas Chale kupitia mradi wa upitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ujulikanao kama ' AIRTEL SHULE YETU'.
 Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kushoto) akimkabidhi vitabu mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Alharamain ya Ilala, mwalimu Nuhu Mruma (kulia) kupitia mradi wa upitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ujulikanao kama ' AIRTEL SHULE YETU'. Katikati ni Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi.
 Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi (kulia) akimkabidhi vitabu mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya White Lake, iliyopo Changanyikeni Jijini Dar es Salaam mwalimu Ignas Fedeo (kushoto) kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ujulikanao kama ' AIRTEL SHULE YETU'. Katikati ni Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU