BODI ya klabu ya soka AZAM FC
imewasimamisha wachezaji wake WATATU , SAID MORAD ,ERASTO NYONI na DEO MUSHI
kwa tuhuma za kupokea rushwa katika mchezo wake dhidi ya SIMBA uliomalizika kwa
AZAM FC kufungwa magoli MATATU kwa MOJA.
Ofisa habari wa AZAM FC,
JAFARI IDD, amesema wachezaji hao wamesimamishwa lengo likiwa ni kupisha
uchunguzi wa tuhuma hizo.
Klabu hiyo itapeleka
taarifa zake kwa chombo maalumu cha dola nchini kuchunguza tuhuma hizo.
0 maoni:
Post a Comment