Thursday, November 22, 2012

KIKOSI CHA CHIPOLO POLO KINATARAJIA KUWASILI DSM TAREHE 16 MWEZI DESEMBA.

Mabingwa watetezi wa Afrika , timu ya taifa ya ZAMBIA , CHIPOLOPOLO itacheza na TAIFA STARS katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kujiandaa na mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Zambia, KALUSHA MBWALYA amesema hivi sasa wameshakubalina na rais wa TFF , LEODIGAR TENGA kuhusiana na mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini DSM DESEMBA 22 mwaka huu.

KALUSHA amesema katika mchezo huo wanatarajia kushirikisha kikosi kizima cha wachezaji, wachezaji wanaochezea ndani ya nchi ya Zambia na wale waanochezea katika mataifa mengine nje ya nchi kujiandaa na mashindano hayo.

Naye balozi wa Tanzania nchini Zambia ,Grace Mujuma amesema mechi hiyo itakuwa chachu kubwa ya kujipima kwa wachezaji wa Tanzania na kutoa fursa kubwa kwa wananchi wa Tanzania kuwaona mabingwa watetezi wa Afrika .

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU