Wednesday, December 19, 2012

AIRTEL WAKISHIRIKIANA NA BARAZA LA VITABU TANZANIA (BAMVITA) WAFANIKIWA KUKUSANYA SHILINGI MILIONI 3 KUCHANGIA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUM

 Mwakilishi wa Bamvita bwana Abdallah Hassan akiwashukuru Airtel Tanzania na watanzania wengine kwa kuweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 3 kwa ajili ya kuchangia elimu kusaidia watoto wenye mahitaji maalum shule za msingi za Uhuru Mchanganyiko, Sinza maalum na Buguruni Viziwi.
 Meneja wa wa Airtel huduma za jamii Bi Hawa Bayumi akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) akitoa shukurani kwa Bamvita na watanzania wote walioshiriki katika kuchangia Elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum wa shule za msingi za Uhuru Mchanganyiko, Sinza maalum na Buguruni Viziwi.
Afisa uhusisano na matukio wa Airtel bi Dangio Kaniki  (katikati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) akitoa shukurani kwa vyombo vya Habari na watanzania ambao wameshiriki kuchangia watoto wenye mahitaji maalum kupitia mradi wa BAMVITA, akifuatiwa kushoto na mwakilishi wa Bamvita bwana Abdallah Hassan na kulia kwake meneja wa wa Airtel huduma za jamii Bi Hawa Bayumi.

Milioni 3 kukabidhiwa kwa shule za watoto wenye uhitaji maalum za jijini Dar es salaam
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilling million 3 kwa ajiri ya kusaidia watoto wenye mahitaji maalum wa shule tatu za msingi za jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Airtel huduma za jamii Bi Hawa Bayumi amesema fedha hizo zitagawanywa katika shule zote tatu na zitatumiika katika manunuzi ya vifaa maalum ambavyo vimeonekana kuwa ni changamoto katika maendeleo ya watoto hao.

 "Airtel Tanzania tunajisikia fahari kushirikiana na Baraza la vitabu Tanzania na  kuwaunganisha watanzania ili kufanikisha dhamira ya kufikisha elimu hata  kwa watu wasiojiweza.  Tunawapongeza BAMVITA kwa kuleta mradi huu ambao umeweza kukusanya jumla ya shilingi milioni tatu, hizi sio pesa ndogo kwa watoto hawa wenye uhitaji kwenye shule hizi za msingi" Bi Hawa Bayumi alisema.

"Hivyo basi Airtel tunawashukuru sana watanzania walioitikia wito na maombi yetu ya kuwachangia watoto hawa walio katika shule hizi zenye uhitaji maalum, tunaomba wote waliojitolea waendelee na moyo huo kwa kuwa kutoa ni moyo na wala sio utajiri, pesa hizi zitatumika kusaidia kununua vifaa vya kufundishia kwaajili ya shule tatu ikiwemo Sinza maalum, Buguruni Visiwi na shule ya msingi Uhuru mchanganyiko zote za jijini dare s salaam" alisisitiza Bi Bayumi.

Kwa upande wake muwakilishi wa BAMVITA  Abdallah Hassan aliwashukuru Airtel na kubainisha kuwa lengo walilojiwekea limeanza kupata majibu mazuri hasa kwa kuona kuna Mashirika pamoja na watu binafsi  wamethubutu kuunga mkono jitihada yao yakuwapunguzia changamoto watoto hao wenye uhitaji maalum wa shule za Uhuru Mchanganyiko, Sinza maalum na Buguruni Viziwi.

Vilevile Afisa Matukio wa Airtel Tanzania alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau mbalimbali pamoja na wanahabari waliojitolea kwa hali na mali kuhakikisha ujumbe wa kuhamasisha wananchi kuchangia mradi huo unawafikia.
 
" Airtel Tunatoa shukurani zetu kwa balozi wetu; Ambwene Yesaya  AY kwa kuweza kushirikiana nasi katika kuwezesha kuchangia katika mradi huu wa Bamvita. Na bila kuwasahau wadau wetu Bw. Issa Michuzi wa Michuzi media Group, Bin Zuberi blog, Father Kidevu blog, Global publisher, Michuz JR na vyombo vyote vya habari na blog zingine zote ambazo kwa kweli waliweka matukio mbalimbali yaliodhamiria kuhamasisha jamii kujitolea kuchanga kwaajili ya watoto hawa wenye uhitaji maalimu" alisema Bi Kaniki
Kampeni hii ya Airtel kushirikiana na Bamvitana imedumu kwa muda wa miezi mitatu  na imefanikiwa kuwawezesha watanzania kuchangia kwa kutuma neno "Vitabu" kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS ilitozwa shilingi 200 na kuingizwa katika mradi huu
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kujitolea katika sekta ya elimu, Airtel mwaka huu tayari imeshajitolea vitabu katika shule za sekondari 93 kupitia mradi wake ujulikanao kama Airtel 'shule yetu',  Shule hizo 93
vile vile airtel imejenga na kukarabati shule ya msingi  Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la DSM kando kando na barabara ya bagamoyo na kuikabidhi kwa Makamu wa Raisi Mh Dkt, Gharib Bilal Novemba  mwaka huu,

Airtel Tanzania bado inaenedelea na mkakati wa kupata shule nyingine itakayofaidika na mradi huo wa kila mwaka kwa kujengwa nakukarabatiwa kuptia mpango huo wa Airtel shule Yetu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU