Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za
kuupokea Mwaka mpya wa Kiislamu 1434 Hijriyya, zilizofanyika katika Ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Desemba 16, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa Kiislamu, baada ya kujumuika
na waumini hao katika sherehe za kuupokea mwaka mpya wa Kiislamu 1434 Hijriyya,
zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Desemba 16,
2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mtoto Mariam Nassor, ambaye ni
miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo kwa mwaka uliopita wa
Kiislma. Makamu alikabidhi zawadi hizo wakati wa sherehe za kuupokea mwaka mpya
wa Kiislamu 1434 Hijriyya, zilizofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam, leo Desemba 16, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Alhad Mussa Salum, akiwa ni mmoja kati ya watu waliofanikisha maandalizi ya
sherehe hizo kuanzia mwaka uliopita wa Kiislma. Makamu alikabidhi zawadi hizo
wakati wa sherehe za kuupokea mwaka mpya wa Kiislamu 1434 Hijriyya, zilizofanyika
katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Desemba 16, 2012.
0 maoni:
Post a Comment