Michuano
ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya
miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inaanza kutimua vumbi kesho
(Desemba 11 mwaka huu) kwenye viwanja viwili tofauti.
Viwanja
vitakavyotumika kwenye michuano hiyo ni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
na Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Viwanja vyote viko Dar es Salaam.
Timu
hizo zimegawanywa katika makundi matatu ya michuano hiyo
itakayomalizika Desemba 23 mwaka huu. Kundi A lina timu za Coastal
Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans.
Kundi
B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba,
wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda
kundi C.
Mechi
za fungua dimba kundi A ni Coastal Union vs Tanzania Prisons (saa 2
asubuhi- Karume), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (saa 10 jioni- Karume). Kundi
B ni African Lyon vs Polisi Morogoro (saa 3 asubuhi- Chamazi) na Azam
vs Mgambo Shooting (saa 10 jioni- Chamazi).
Kundi
C litaanza mechi zake Desemba 12 mwaka huu ambapo Kagera Sugar itacheza
na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting
zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.





0 maoni:
Post a Comment