Tuesday, December 18, 2012

SIKU YA WANAFAMILIA WA NBC ILIVYOFANA DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (katikati) akizungumza na wafanyakazi na familia zao katika sherehe za Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi. Wengine ni viongozi wa ngazi za juu wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru akiwania mpira pamoja na mfanyakazi wa benki hiyo, katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
 Wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakishindana kuvuta kamba ili kumpata mshindi katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
  Watoto wa wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania wakishindana kufukuza kuku ili kumpata mshindi katika sherehe ya Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
 Wafanyakazi na familia zao wakiselebuka katika sherehe za Siku ya Wanafamilia wa NBC jijini Dar es Salaam juzi.
  Hapa watoto wakionyeshana nani ni mkali katika kusakata muziki kwa kutumia mtindo maarufu ujulikanao kwa jina la ‘Kiduku’ uliofanya sherehe hizo kunoga zaidi.
Father Christmas’ akigawa zawadi kwa watoto wa wafanyakazi wa benki ya NBC Katika sherehe ya Siku ya wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU