Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah akizungumza na waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi TFF
Shirikisho La soka nchini TFF limesikitishwa kwa timu za TAIFA ZA TANZANIA KILIMANJARO STARS
na ZANZIBAR HEROUS kutolewa katika hatua
ya nusu fainali ya michuano ya TUSKER CHALLENGE CUP inayofanyika nchini UGANDA.
Katibu mkuu wa TFF ANGETILE OSIAH amesema
walitengemea timu hizo zingefika fainali lakini kutoka na timu pinzani kuwa na
wachezaji wenye uzoefu mkubwa timu hizo zimeshindwa kufika hatua ya
fainali,lakini TFF inajipanga kuhakikisha anawalea vijana ili baadaye weweze
kufanya vizuri.
Katika michuano hiyo KILIMANJARO STARS ilitolewa na
UGANDA baada ya kufungwa magoli matatu kwa bila katika hatua ya nusu fainali
,sawa na ZANZIBAR HEROUS ambayo nayo ilitolewa na KENYA kwa njia ya matuta .
Mashindano hayo yanatarajia kumalizika kesho kwa
ZANZIBAR na TANZANIA kucheza kutafuta mshindi wa tatu wakati fainali itakuwa
kati ya KENYA na UGANDA.





0 maoni:
Post a Comment