TIMU za TANZANIA za KILIMANJARO STARS na ZANZIBAR
HEROES zimeshindwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya CECAFA CHALENJI
baada ya kuondoshwa katika mashindano hayo na timu za KENYA na wenyeji UGANDA.
Katika mchezo wa awali , ZANZIBAR HEROES iliweza
kucheza vizuri katika mchezo wake dhidi ya HARAMBEE STARS ya KENYA na
kushuhudia mchezo huo ukimalizika hadi dakika MIA na ISHIRINI zikiwa sare ya
kufungana magoli MAWILI kwa MAWILI.
Mchezo huo ukaamuliwa kwaa penati ambapo HARAMBEE
STARS ilipata penati NNE na ZANZIBAR ikapata penati MBILI na hivyo kuondolewa katika
mashindano haya.
Katika mchezo wa pili, Wachezaji EMMANUEL OKWI na
ROBERT SSENTONGO walipeleka kilio kwa
timu ya KILIMANJARO STARS baada ya kuifungia timu yao magoli matatu kwa bila.
Kutokana na matokeo haya timu za TANZANIA za
KILIMANJARO STARS na ZANZIBAR HEROES zitakutana katika mchezo wa kutafuta
mshindi wa TATU wakati UGANDA na KENYA
zitakutana katika mchezo wa fainali






0 maoni:
Post a Comment