Timu ya Azam FC kesho Jumanne itamalizia ziara yake
ya mechi za kirafiki jijini Nairobi kwa kucheza dhidi ya K.C.B kwenye Uwanja wa
City.
Azam FC iko jijini hapa kwa ziara ya maandalizi kwa
ajili ya ligi kuu na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, imecheza michezo
miwili, imefungwa 2-1 na AFC Leopards na ikashinda mchezo mmoja 1-0 SOFAPAKA.
Ziara hiyo ya siku saba inamalizika leo kwa mchezo
huo ambapo kikosi hicho kitarejea jijini Dar es Salaam, siku ya Jumatano tayari
kwa mechi za ligi kuu.
Katika ziara hiyo hadi jana jioni wachezaji wote
walioko safarini wamecheza katika michezo hiyo miwili akiwepo kipa namba mbili
Aishi Salum.
Akizungumzia mchezo wake wa mwisho, kocha Stewart
alisema wachezaji wote wako safi kwa mchezo huo kwa kuwa hakuna majeruhi yoyote katika michezo
hiyo.
Alisema wakimaliza mashindano hayo watakuwa
wamejiimarisha vya kutosha kwa ligi kuu, wachezaji watakuwa imara na
kurekebisha makosa yao.
“Mechi na KCB tutacheza tukiwa safi, tumepumzika
siku moja, wachezaji wamepata mapumziko, itakuwa mechi nzuri” alisema Stewart.
Mchezo huo utachezwa kwenye kiwanja cha City ambacho
ni cha nyasi bandia sawa na kile cha Azam Complex Chamazi.
0 maoni:
Post a Comment