Licha ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki
dhidi ya A.F.C Leopard, kocha wa Azam FC Stewart Hall amesema timu yake
imecheza vizuri na kufungwa ni sehemu ya mchezo.
Stewart alisema haikuwa bahati kwao kwa kuwa
walipata nafasi nyingi za wazi umaliziaji ukawa tatizo, pia na penati mbili
walizopata wachezaji wake walikosa na kuipa ushindi timu hiyo ilikuwa na
mashabiki wengi uwanjani hapo.
“Timu inayocheza vizuri ni ile inayotengeneza nafasi
na kucheza mpira mzuri, tulicheza vizuri nafurahi kuona wachezaji wanajituma,
kukosa penati na nafasi za wazi ni matatizo yanaweza kuzibika” alisema Stewart
Aliongeza kuwa kupitia mechi hizi zote watakuwa na
wakati mzuri wa kurekebisha makosa yanayotokea kabla ya kuanza kwa mechi za ligi.
Katika mchezo huo AFC walikuwa wa kwanza kupata
magoli yalifungwa katika dk ya 14 na Paul Were na dk 54 Mike Baraza aliifungia
timu hiyo goli la pili kufuatia kosa la beki wa Azam FC, David Mwantika
kumruhusu akapiga shuti likaenda moja kwa moja wavuni.
Azam FC walipata penati tatu katika dk 19, Jockins
Atudo alikosa baada ya kupiga mkwaju uliotoka nje, dk 65 Khamis Mcha nae
alikosa penati baada ya kugonga mwamba na kurudi ndani ikaokolewa na mabeki wa
AFC.
Goli la Azam FC lilipatikana kupitia kwa mkwaju wa
penati iliyopigwa na Samih Haji Nuhu baada ya beki wa AFC Erick Masika
kumwangusha Humprey Mieno kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili Kocha Stewart alifanya mabadiliko
walitoka, Luckson Kakolaki, Salum Abubakar, Abdulhalim Humud, Uhuru Seleman, Jabir
Aziz na Gaudence Mwaikimba nafasi zao zikachukuliwa na David Mwantika, Michael
Bolou,Humphrey Mieno, Ibrahim Mwaipopo, Brian Umony na Abdi Kassim, mabadiliko
hayo yaliimarisha kikosi hicho muda wote wa mchezo.
Baada ya mchezo huo kocha wa AFC, Tom Olaba alisema kupata
ushindi kwa kuifunga timu bora ni mafanikio kwake na kuonyesha ukomavu kwa
wachezaji wake.
“Unajua Azam FC ni timu nzuri, tulijiandaa na
kupanga kikosi ambacho kitapambana na timu hiyo, nimefurahishwa na ushindi huo
kwa kuwa nina wachezaji wapya saba katika timu yangu na wamecheza vizuri na
kushinda” alisema Olaba.
Azam FC leo Jumapili jioni itacheza mechi ya pili
dhidi ya SOFAPAKA kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, kesho itapumzika na
kufanya mazoezi katika Uwanja wa City kabla ya kucheza na KCB katika Uwanja huo
siku ya Jumanne.
Azam FC Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu,
Luckson Kakolaki/David Mwantika 45’, Jockins Atudo, Jabir Aziz/Humphrey Mieno
45’, Salum Abubakar/Ibrahim Mwaipopo 45’, Abdulhalim Humud/Michael Bolou 45’,
Uhuru Seleman/Brain Umony 45’, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim 60’ na Khamis
Mcha.
AFC Leopards Martin Musaliya, Edwin Mafula, Noah
Abichi, Erick Masika, Antony Kimani, Martin Imbalambala/Michael Wendera, Benard
Mangoli/Benard Ongoma, Patilah Omoto, Victor Ochieng/Edward Seda, Mike Baraza/Noah
Wafule na Paul Were
0 maoni:
Post a Comment