
Bondia Gottlieb Ndokosho akiunyanyua mkanda wa IBF baada ya kumtwanga Maoja
Bondia Gottlieb Ndokosho kutoka nchini Namibia
ambaye alimchapa kwa KO bondia Rajabu Maoja wa Tanzania atapanda tena uliongoni
February 2, 2013 katika jiji la Windhoek, nchini Namibia kupambana na bondia
Prosper
Ankrah kutoka nchini Ghana.
Wawili hao watapambana katika mpambano wa mwaka wakati
Ndokosho wakati atakapotetea mkanda wa IBF wa bara la Afrika,
Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika uzito wa unyoya.
Ndokosho aliupata mkanda huo tarehe 29 Septemba 2012 wakati
alipomshinda Mtanzania Rajabu Maoja katika mpambano uliofanyika
katika ukumbi wa SPK jijini Windhoek, nchini
Namibia.
Mpambano mwingine wa IBF katika bara la Africa siku hiyo nchini
Namibia utawakutanisha mabondia Albinus Felesianu wa Namibia
atakapopambana na bondia Asamoah
Wilson kutoka nchini Ghana katika uzito wa Super
Featherweight.
Wakati huo huo bondia
mkali wa Tunisia Ayoub Nefzi mwenye
makao yake nchini Belgium atapambana na bondia Ishmael Tetteh wa Ghana kugombea mkanda
wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF
AMEPG).Mpambano huo utafanyika February 15 katika jiji la Tunis nchini
Tunisia.
Bondia anayekuja juu kwa kasi wa Ghana Richard
Commey atachuana na Mgahana mwenzake Bilal Mohammed
kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya
Uajemi.
Mpambano huu utafanyika sambamba na ule utakaowakutanisha Mtanzania
Fadhili Majia na Isaac Quaye wa Ghana.
Mtanzania mwingine Allen Kamote atapimana nguvu na bondia
machachari na bingwa wa WBA wa mabara
Emmanuel Tagoe wa Ghana siku hiyo hiyo tarehe 22 February.
Naye bondia mwana dada Helen Joseph wa Nigeria atapambana na
bondia Mariana Gulyas wa Hungary
kugombea mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Unyoya. Mpambano wa wanadada
hao utafanyika katika jiji la Accra, nchini Ghana tarehe 30 mwezi wa March,
2013.
Hili litakuwa pambano la kwanza kwa bondia Helen Joseph tangu apoteze pambano la
IBF la ubingwa wa dunia nchini Dominican Republic alipokutana na bondia Dahianna Santana wa Domoinican
Republic.
Mapambano hayo yote yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo
Ngowi.
0 maoni:
Post a Comment