Wednesday, January 16, 2013

MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI

 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya
Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akifurahia jambo na Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya leo (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
Picha na Tume ya Katiba.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU