Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Mary Kashonda na Dkt.
Sengondo Mvungi wakifuatilia mkutano kati ya Tume na Jumuiya ya Kidini
ya Khoja Shia Ithnaasher Jamaats uliolenga kupata maoni ya taasisi hiyo
kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini
Dar es Salaam leo (Ijumaa, Jan 11, 2013).
Mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Kidini ya Khoja Shia Ithnaasher Jamaats Bw. Mohamed Khalfan akitoa
maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam leo (Ijumaa Januari 11, 2013).
Mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Kidini ya Khoja Shia Ithnaasher Jamaats Bw. Mohamed Dhirani akitoa
maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam leo (Ijumaa Januari 11, 2013).
Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA),
Kanda ya Mashariki Mchungaji Mark Malekana (kushoto) akitoa maoni ya
kanisa lake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam leo
(Ijumaa Januari 11, 2013).
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Kanda ya Kusini, Dk. Joseph Bulongela akitoa akitoa maoni ya taasisi yake kuhusu kuhusu
Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika
katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa Januari 11,
2013).
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani akizunguma na viongozi Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) (kushoto) katika mkutano uliolenga kupata maoni ya kanisa hilo kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa Januari 11, 2013).
Sheikh Ibrahim Ghulaam wa Baraza Kuu
la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini akitoa maoni ya Baraza hilo
kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa wa Karimjee Jijini Dar es
Salaam leo (Ijumaa tarehe 11, Januari, 2013).
0 maoni:
Post a Comment