Wachezaji na bechi la ufundi la timu ya Young Africans
wamefurahishwa na hali ya kambi hapa katika mji wa Antalya kwamba hali
ya hewa ni nzuri, vyakula aina zote vinapatiikana na huduma za mazoezi
kwa ajili ya kambi ni za kiwango cha juu sana.
Wakiongea na www.youngafricans.co.tz
Kocha wa makipa Razaki Siwa amesema kw akeli hali ya hewa sio mbaya
kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali, hali ya hewa ni nzuri, mazingira
ya kambi ni ya kuridhisha vifaa vya kwa ajili ya mazoezi vipo kwa wingi
hivyo inakuwa nio rahisi kwetu walimu kuwaelekeza wachezaji wafanye
nini.
Kocha
Siwa amesema pia wanaushukuru uongozi wa Young Africans kwa kuamua
kuileta timu kambini nchini Uturuki kwani wachezaji wanapata nafasi
nzuri ya kujifunza kwa pamoja, mafunzo ambayo hayana bughuza kwani kambi
ipo katika hadhi ya kimataifa ndio maana timu nyingi za Ulaya zinapenda
kuja kuweka kambi eneo tulivu kama hili la Antalya.
Fred
Felix Minizro kocha msaidizi kwa upande wake amesema hali ya kambi kwa
ujumla ni nzuri, na kuhusu hali ya hewa ni baridi ya kisai tu kama Mbeya
na Arusha hivyo haoni kama hali ya hewa inaweza kuwa ni kikwazo katika
kambi hii ya mafunzo.
Naye kiungo
mshambuliaji Saimon Msuva amesema wanafurahia kupata nafasi hii ya kuja
kuweka kambi nchini Uturuki, kwani anaamin mazingira na huduma z akambi
ni nzuri kabisa hivyo wanayapokea vizuri mafunzo ya kocha mkuu Brandts
na pindi watakaporudi Tanzania wataweza kuwapa raha wapenzi wa soka kwa
kuwaonyesha ni nini hasa wamekipata kwa kipindi cha wiki mbili.
0 maoni:
Post a Comment