
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazitakia kila la kheri timu za
Azam, Jamhuri na Simba ambazo zinaiwakilisha Tanzania katika michuano ya
Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
Azam
inacheza na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini katika mchezo wa Kombe la
Shirikisho utakaofanyika Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Nayo
Jamhuri ya Zanzibar kesho itacheza na St. Georges ya Ethiopia katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Uwanja wa Gombani
kisiwani Pemba. Simba itacheza na Recreativo do Libolo ya Angola
keshokutwa (Februari 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
CAF YASITISHA UKAMISHNA WA HAFIDH ALI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limesitisha ukamishna wa Hafidh Ali.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika iliyokutana Januari 17 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika
Kusini.
Kwa
mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani kwa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ukamishna huo umesitishwa kwa vile
hadi sasa Shirikisho hilo halijapata ripoti ya mechi namba 78 kati ya
Comoro na Libya ambayo Ali aliteuliwa kuisimamia.
Hivyo,
ukamishna wa Ali umesitishwa hadi hapo CAF itakapopokea ripoti
kuhusiana na mechi hiyo ambayo ilikuwa ni kutafuta tiketi ya kucheza
Fainali za AFCON zilizofanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini.
0 maoni:
Post a Comment