Mechi
namba 119 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 13 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka
ushindi wa mabao 4-0 imeingiza sh. 68,438,000.
Watazamaji
12,147 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 16,170,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 10,439,694.92.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 10,982 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 54,910,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 8,222,162.26,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,933,297.36, Kamati ya Ligi
sh. 4,933,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,466,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,918,504.53.
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA TASMA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) uliochaguliwa
katika uchaguzi uliofanyika Februari 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TASMA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia tiba ya wanasoka nchini.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TASMA
chini ya uenyekiti wa Dk. Mwanandi Mwankemwa aliyeibuka mshindi katika
uchaguzi huo kwa kura 18 dhidi ya 7 za aliyekuwa Mwenyekiti Biyondho
Ngome
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba ya TASMA pamoja na
vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TASMA chini ya Dk. Paul
Marealle na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo
unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu
nzima ya uongozi wa TASMA iliyochaguliwa inaundwa na Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Mwenyekiti), Dk. Nassoro Matuzya (Katibu Mkuu), Sheky
Mngazija (Katibu Msaidizi), Dk. Juma Mzimbiri (Mhazini), Joakim Mshanga
(mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF) na Dk. Hemed Mziray (mjumbe wa Kamati ya
Utendaji).
Ukiondoa
nafasi ya Mwenyekiti, wagombea wengine wote hawakuwa na wapinzani.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti haikupata mgombea, hivyo itajazwa katika
uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment