Wednesday, February 27, 2013

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia makamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yao February 27, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU