Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal
Lesoinne (kushoto), akikabidhi mfano wa hati kwa mmoja wa wasambazaji
wa saruji ya TPCC, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwanza Huduma Co
Ltd, Zully Manji baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa jumla wa
wasambazaji bora wa saruji ya Twiga, katika hafla ya Usiku wa
Wasambazaji wa Twiga Cement jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo.
Alipewa zawadi ya tani 40 za saruji.
Baadhi ya wasambazaji wa saruji ya Twiga na wafanyakazi wa TPCC
wakiselebuka katika hafla hiyo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal
Lesoinne (kushoto), akikabidhi mfano wa hati kwa Mkurugenzi wa
kampuni ya V.G.K Ltd, Valence Msack kama uthibitisho wa zawadi ya tani
25 za saruji iliyopewa kampuni hiyo baada ya kuibuka mshindi wa tatu
wa wasambazaji bora wa saruji za Twiga, katika hafla ya Usiku wa
Wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Twiga, Pascal Lesoinne
(kushoto), akikabidhi cheti cha shukrani kwa mmoja wa wasambazaji wa
saruji ya TPCC, Bi. Chaba Mavura ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Samks Traders Ltd, katika hafla ya Usiku wa Wasambazaji wa
Twiga Cement jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga, Ekwabi Majigo.
0 maoni:
Post a Comment