Yanga
na Mtibwa Sugar zinapambana kesho (Februari 2 mwaka huu) katika moja ya
mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Mwamuzi
Ronald Swai kutoka Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo
inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza ligi
hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mechi iliyopita walilala mbele
ya Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa ligi kwa sasa.
Polisi
Morogoro itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Jamhuri,
mjini Morogoro wakati Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji
wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ruvu Shooting inayofundishwa na
Charles Boniface Mkwasa.
Keshokutwa
(Jumapili) kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal
Union katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.





0 maoni:
Post a Comment