Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaipongeza klabu ya Azam kwa ushindi
wa mabao 2-1 ilioupata timu yake katika mechi ya raundi ya kwanza ya
michuano ya Kombe la Shirikisho.
Mechi
hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ilichezwa jana jijini
Monrovia, na timu hizo zitarudiana wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ushindi
huo unaiweka Azam chini ya kocha wake Stewart John Hall katika
mazingira mazuri ya kusonga mbele baada ya mechi ya marudiano. Bila
shaka ushindi wa timu ya Azam pamoja na mambo mengine umechangiwa na
klabu hiyo kujipanga vizuri.
Hata
hivyo ushindi huo bado ni changamoto kwa wachezaji, benchi la ufundi na
uongozi wa Azam kuhakikisha unajipanga vizuri kwa mechi ya marudiano
kwa vile mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu; kushinda, kutoka sare
au kufungwa.
Msafara
wa timu ya Azam unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF,
Blassy Kiondo unatarajiwa kurejea nchini kesho alfajiri kwa ndege ya
Kenya Airways kupitia Nairobi.
0 maoni:
Post a Comment