Mkurugenzi wa QS Mahonda, katikati, akiwa na Martha Mwaipaja kulia.
Stara akiwa na wakali wa kwaya
MKURUGENZI wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph Mhonda,
amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa tamasha lao la ‘Tumaini Jipya’
linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, linagusa hisia za wengi kwa
kushirikisha wakali mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mhonda alisema kuwa
alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na
kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani
Morogoro.
“Tamasha hili limeanzia Morogoeo lakini litaendelea kwenye m
ikoa mingine ya Tanzania likiwa na lengo
la kutoa tumaini kwa jamii, na mapato
yatakayopatikana yatasaidia watu walio
katika mazingira magumu” alisema Mhonda
Alisema katika tamasha hilo ambalo ni la aina yake kufanyika
Tanzania, litapambwa na waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki
ambao ni Bahati Bukuku,
Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki,
Stara Thomas, Matha Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven.
Mbali na waimbaji hao
pia kutakuwa na kwaya mbalimali Rafiki Gospel Singers, Haleluya Kwaya,
Victoria Kwaya na MTC .
Mhonda alisema sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia
waimbaji hao pia watakuwa na muda maalum wa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa
watu wote, pamoja na mbinu za kufaulu mtihani kwa wanafunzi.
Kwa mujibu wa waandaaji hao, Tamasha la Tumaini Jipya, ni fursa
pekee kwa wakazi wa Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika
kusherehekea siku Kuu ya Pasaka.
0 maoni:
Post a Comment