HATMA
ya African Lyon kuendelea kushika mkia au la kwenye Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) inajulikana kesho wakati itakapokuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting
kwenye Uwanja Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Lyon
yenye pointi 13 kutokana na mechi 19 inabidi iifunge Ruvu Shooting kama
inataka kuirejesha mkiani Toto African yenye pointi 14. Kama kweli
inazitaka pointi zote tatu itabidi ifanye kazi mbele ya Ruvu Shooting
inayotiwa makali na Kocha Charles Boniface Mkwasa.
Hiyo
itakuwa mechi ya 18 kwa Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya saba ikiwa
na pointi 26 ikitanguliwa na vinara wa ligi hiyo Yanga, Azam, Simba,
Coastal Union, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar yenye pointi 28 ikinolewa na
nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Maxime.
Mechi
hiyo namba 139 itachezeshwa na mwamuzi Amon Paul kutoka Musoma wakati
wasaidizi ni Anold Bugado wa Singida na Milambo Tshikungu kutoka Mbeya.
Mwamuzi wa mezani atakuwa Shafii Mohamed wa Dar es Salaam.
Nayo
Tanzania Prisons ya Jumanne Chale itakuwa mgeni wa Oljoro JKT katika
mechi itakayochezwa Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha
wakati Mgambo Shooting itaoneshana kazi na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Keshokutwa
(Machi 7 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya JKT Ruvu ya Kocha Charles Kilinda na Kagera
Sugar.
Ligi
hiyo itaendelea tena Jumamosi ya Machi 9 mwaka huu kwa mechi mbili;
Yanga vs Toto Africans (Uwanja wa Taifa), na Azam vs Polisi Morogoro
(Azam Complex, Chamazi).
0 maoni:
Post a Comment