Badhi Ya Washiriki Wa Miss Utalii , Wakitembelea Hifadhi
Ya Taifa Ya Tarangire
Washiriki Washiriki Wa Miss Utalii Tanzania, Wakifundisha
Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Bagamoyo, Walipotembelea Shule Hiyo
Mkuu Wa Hifadhi Ya Tarangire Erasto Lufungilo Akizungumza
Na Washiriki Wa Miss Utalii Walio Tembelea Hifadhi Hiyo
Fainali
za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13, zilizo kuwa zimepangwa
kufanyika 17,machi 2013 katika ukumbi wa
Dar Live Dar es Salaam, zimesogezwa mbele hadi tarehe 30-3-2013,katika ukumbi
utakao tangazwa badae. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Rais wa Mashindano hayo nchini na Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo,
alisema kuwa sababu ya kuahilishwa kwa
fainali ni pamoja na upungufu wa bajeti ,uliosababishwa na baadhi ya wadhamini
wakubwa walio ahidi kushindwa kutimiza
ahadi zao kama walivyo ahidi, hivyo kupelekea upungufu wa zaidi ya shilingi
170,000,000/= , kati ya bajeti ya shilingi 870,000,000/= zinazohitajika ili
kukamilisha fainali hizo.
“Ili kulifanya shindano hili kwa ubora na kiwango cha kimataifa, tunahitaji sio chini ya shilingi 870 Milioni, ambapo hadi sasa tumefanikiwa kupata jumla ya shilingi 600Milioni, na tunaupungufu wa jumla ya shilingi 170 Milioni, ambao umesababishwa na baadhi ya wadhamini , kushindwa kutimiza ahadi zao kulikotokana na matatizo mbalimbali waliyo yapata ya kibiashara. Mashindano haya kama yalivyo mashindano mengine nchini na Duniani yanategemea udhamini kutoka kwa sekta binafsi na za umma, kwani gharama za kuyaendesha na kuyaandaa mashindano haya ni kubwa,ambazo haziwezi kulipwa wala kufidiwa kwa kutegemea viingilio vya getini”.
Hali
hii imetulazimu kuahilisha fainali hizi hadi 30-3-2013,ili kupata muda wa
kupata kiasi hicho cha fedha, na kukamilisha maandalizi kwa ubora na viwango
vya kimataifa. Taratibu za kupata fedha hizo zinakaribia kukamilika kabla ya
tarehe ya shindano kutoka kwa wadau wa utalii katika sekta binafsi na za umm.
Kambi ya washiriki inaendelea katika hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam,
ambapo kuanzia jumanne tarehe 19-3-2013 , washiriki wote wakiambatana na
waandishi wa habari, wataanza ziara ya wiki moja katika hifadhi za Taifa za
Mikumi,Saadani na Udzungwa, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Udizungwa
washiriki watapanda milima ya udizungwa hadi katika kilele cha Maporomoko ya
maji ya Sanje , ambayo ni kivutio kikubwa katika hifadhi hiyo.
0 maoni:
Post a Comment