Wednesday, March 13, 2013

MWANADADA HELEN JOSEPH AKWEA KILELE CHA UBINGWA WA IBF

 Helen Joseph, bondia mwanadada ambaye anaishi katika jiji la Accra, nchini Ghana akipigana ngumi yuko mboni kupanda kilele cha mafanikio katika maisha yake ya ngumi. Ni wakati ambao Helen Joseph anayetoka katika nchi ya Nigeria aliokuwa anaungojea katika maisha yake ya ngumi.
Mwaka jana alikutana na bondia Dahianna Santana katika jiji la San Domingo, nchini Dominican Republic kugombea ubingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa Unyonya (Fearherweight). Taabu na kashikashi zote alizozipata wakati wa patashika ile ya mwaka jana zimekuwa fundisho tosha kwa Helen wakati anapojiandaa kukutana na Marianna Gulyas kutoka nchini Hungary kugombea ubingwa wa IBF wa mabara katika uzito wa unyoya.
Mpambano huo, unaoandaliwa na kampuni maarufu ya kukuza ngumi ya GoldenMike Boxing Promotion Syndicate ya nchini Ghana unategemea kuwa wa patashika kweli kutokana na mabondia wote wawili kuwa na ujuzi tele ulingoni. Wawili hawa watakutana tareeh 30 March katika uwanja wa michezo wa Accra na mpambanohuu utarushwa moja kwa moja na luninga ya Super Sports.
Ni mapromota wachache na mameneja wachache  ambao wanaweza kuwekeza kiasi kikubwa hivyo cha pesa katika mchezo wa ngumi namna ambapo kampuni ya GoldenMike Boxing Promotions Syndicate ya nchini Ghana imewekeza katika kuinua kipaji cha mwana dada Helen Joseph.
Kwa upande wake Helen ambaye ni nadhifu, mtanashati na mwenye nidhamu ya hali ya juu, mchezo wa ngumi ndio unaomlisha katika maisha yake na atatumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa taji hli kubwa la ngumi linabaki barani Afrika na kulitumia kama ngazi ya kukutana tena na Dahianna Santana katika ubingwa wa dunia!

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU