Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
ameipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa mabao 2-1 ilioupata timu yake
katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Mechi
hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ilichezwa jijini Monrovia,
matokeo ambayo yanaweka Azam katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada
ya mchezo wa marudiano utakaofanyika wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Amesema
Azam imefanya jambo kubwa, kwani kushinda ugenini hasa katika nchi za
Afrika Magharibi si jambo dogo, hivyo Watanzania waendelee kuiunga mkono
na anaitakia kila la kheri katika mashindano hayo.
0 maoni:
Post a Comment