Jaji Mkuu wa shindano la Safari lager Nyama choma, Douglas Sakibu
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
vigezo watakavyovitumia kuamua nani mshindi wa shindano hilo kwenye
ukumbi wa TBL Mwanza jana.Katikati ni Menej wa Bia ya Sfari Lager, Oscar
Shelukindo na Meneja Mauzo na usambazaji wa Kanda ya Ziwa, Malaki
Sitaki.
Fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa mwanza zinatarajiwa kufanyika kesho katika
Viwanja vya Furahisha kwa udhamini wa
TBL, kupitia Bia yake ya Safari Lager
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza Meneja wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo alizataja Bar tano zilizofanikiwa kuingia fainali kuwa
ni Victoria Prince ya CCM Kirumba,AR ya Nyakato,Shokeni ya Mkuyuni na Shooters
ya Kirumba ndizo ambazo zitashindana na kumpata nani bingwa wa kuchoma nyama kwa
mkoa wa Mwanza katika mashindano hayo yajulikanayo kwa “Safari Lager Nyama
Choma Competition 2013”
Alisema Shelukindo fainali hizo zitasindikizwa na burudani ya Mziki
kutoka kwa Bend ya Africana Music na wasanii mbalimbali ikiwemo ngoma za asili.
Shelukindo alisema, “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma
ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja
waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa nyama choma.
Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata
elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili
kila anapokula nyama choma. Tumezingatia maombi ya washiriki mwaka jana hivyo
basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama ilitafanyika
kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama
ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Bwana Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba,
washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu;
nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.
Kiongozi wa
jopo la majaji ambao ni wataalamu maarufu nchini katika tasnia hii, bwana
Douglass Sakibu alielezea kwamba majaji wataangalia kwa makini sana vigezo
mbalimbali katika utayarishaji wa nyama choma. Alitaja baadhi ya vigezo hivyo
kwamba ni usafi, vifaa vya kufanyia kazi, joto maalum la uchomaji nyama nk.
Bwana Sakibu aliendelea kusema kwamba, “Tynawaomba wakazi wa Mwanza wajitokeze
kuja kula nyama Bora na kushuhudia Bar bora itakayoshinda katika fainali hizo
jumapili katika viwanja vya Furahisha
Nae Meneja
Mauzowa na usambazaji wa Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki alizitaja zawadi kwa
mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja,wa pili laki
nane,watatu laki sita ,wanne laki nne na wa tano lai mbili.
Malaki
alilisisitiza kuwaomba wakzi wa Mwanza wajitokeze kwenye fainali hizo
Washuhudie Bar
bora kwa kuchoma nyama na kupata burudani bure kwani hapatakuwa na kiingilio
chochote.
0 maoni:
Post a Comment