Mkuu wa Wilaya wa Rungwe Mkoani Mbeya,Chrispin Meela (kulia)akimkabidhi
kitita cha shilingi milioni moja Mpishi Mkuu wa Bar ya Saigon, Joseph
Aluta mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya
Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya
CCM Iromba mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mkurugenzi wa Bar ya Saigon,
Ally Mohamed na Meneja Mauzo wa rejareja wa Mkoa Mbeya, Michael Myinga
Wafanyakazi wa Bar ya Saigon na mashabiki wakishangilia huku wakiwa
wamembeba mpishi Mkuu wa Bar hiyo,Joseph Aluta mara baada ya kuibuka
mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma Mkoa
wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Iromba mwishoni mwa wiki.
SAIGON
Pub, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa Mbeya, baada
ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya mashindano hayo
yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari
Lager.
Kwa
kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika juzi Jumapili kwenye
Uwanja wa CCM Ilomba, baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja
pamoja na cheti.
Waliokuwa
mabingwa watetezi wa mashindano hayo mkoani hapa, New City Pub,
walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha Sh 800,000 na cheti,
wakati Mbeya Carnival walishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh
600,000 na cheti.
Walioibuka
na nafasi ya nne ni baa ya Nebana iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti,
wakati baa ya Chabruma ilishika nafasi ya tatu na kuzawadiwa Sh 200,000
na cheti.
Akizungumza
kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu,
alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa
kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja
vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na
mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa
vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager
kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani hapa kabla ya kuhamia mikoa
mingine.
“Tulianza
kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika
shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Mbeya tukapata baa hizi tano
zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.
“Tunajua
watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama hivyo tukaona ni vema
tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate nyama bora,”
alisema.
Alisema
kuwa bia ya Safari Lager ina miaka takriani 36 na bado imeendelea
kuwapo hadi sasa ambapo Mbeya ndio inayoongoza kwa mauzo ya bia hiyo
miongoni mwa mikoa yoye ya Tanzania.
Kwa
upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin
Meela, aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo,
akisema kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga
uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool
Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika michezo
mbalimbali kama soka na mingineyo.
“Mashindano
haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa nyama mazingira mazuri na
salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,” alisema.
Alizitaka
baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa na badala yake kujipanga
kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha yale waliyokosea
mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment