Kampuni ya Kinda Boxing Promotions ikishirikiana na kampuni ya Warriors Promotions CC zote za Namibia
leo waliitisha mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya Mieleka
na Ngumi ya Namibia kulitangaza pambano kati ya bondia Albinus Felesianu wa Namibia
na Herbert Quartey wa Ghana.
Mpambano huo wa kugombea mkanda
wa ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana katika uzito wa Super Featherweight,
utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Windhoek
Country Club and Casino tarehe 29, Machi mwaka huu na linatagemewa kuwa
pambano kubwa lililowahi kutokea katika nchi ya Namibia.
Wageni rasmi na muhimu waliohudhuria
mkutano huo ni pamoja na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati Mtanzanai Onesmo Ngowi pamoja na bwana Oiva Angula ambaye ni
Meneja Mkuu wa kampuni ya Simu ya Telecom nchi Namibia.
Rais
Ngowi aliahidi ushirikiano
wa IBF katika kukuza ngumi katika nchi ya Namibia na kuihamashisha
serikali ya
nchi hiyo kuwa pamoja na uwekezaji inaoufanya kwa sasa ni muhimu pia
iwekeze
zaidi katika kujenga na kuendeleza miundombinu endelevu ya mchezo wa
ngumi. Ngowi
aliihakikishia nchi ya Namibia kuwa IBF daima itakuwa mshirika wa karibu
katika
maendeleo ya ngumi ya Namibia. Rais Ngowi yuko nchini Nmibai kusimamia
pambano la ngumi la ubingwa wa kimataifa katika uzito wa Bantam kati ya
bondia Immanuel “Prince” Naidjala wa Namibai na Lesley Sekotswe kutoka nchini Botswana litakalofanyika leo saa moja unusu usiku katika ukumbi wa Windhoek Country Club and Casino.
Naye meneja wa Telecom Namibia bwana
Angula alitangaza rasmi mpango kabambe wa kuijenga uwezo tasnia ya ngumi ya Namibia
kwa kugawa vifaa vya mchezo huo kwa wadau mbalimbali pamoja na kujenga uwezo
kiufundi kwa wale wote wanaosimamia mchezo wa ngumi nchini Namibia kwa sasa.
Bwana Angula alimhakikishia Rais
Ngowi kuwa Telecom Namibia daima itakuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo
ya ngumi nchi humo!
Albinus Felesianu anakuwa bondia
wa kwanza kutoka Namibia kugombea mkanda wa dunia wa IBF na hii inaleta hamasa
kubwa katika taifa hili la watu wapatao milioni mbili na ushee!
0 maoni:
Post a Comment