Thursday, March 7, 2013

TFF WAKABWA KOO NA WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO

 
KIKAO kati ya wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo , Baraza la michezo la Taifa BMT na shirikisho la soka nchini TFF kimefanyika jijini DSM leo ambapo maadhimio matatu yametakiwa kukubaliwa au la na TFF kabla ya jumatatu wiki ijayo.

Katika kikao hicho, WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI na MICHEZO iliwakilishwa na waziri FENELLA MUKANGARA, naibu waziri wizara hiyo AMOSI MAKALA, Katibu wa wizara hiyo na mkurugenzi wa michezo.

Kwa upande wa BMT , yenyewe iliwakilishwa na Mwenyekiti wa baraza hilo , DIONIZ MALINZI na Katibu wa baraza hilo ,

Wakati ujumbe kutoka shirikisho la soka nchini TFF uliwakilishwa na SUNDAY KAYUNI ambaye alimwakilisha rais wa shirikisho hilo, LEODIGAR TENGA, Katibu mkuu wa TFF, ANGETILE OSIAH na ALEX MGONGOLWA.

Baadhi ya maamuzi ya serikali kwenda TFF ni pamoja kutoa siku THEMANINI ambapo TFF imetakiwa kufanya mkutano mkuu wa marekebisho ya katiba yake katika siku zisizozidi AROBAINI yaani hadi tarehe 15 ya mwezi ujao.

Jingine ni pamoja na kuhakikisha uchaguzi wa shirikisho hilo unafanyika katika kipindi cha siku arobaini yaani kuanzia siku ya tarehe 15 ya mwezi ujao ambapo hadi Mei 25 shughuli za uchaguzi ziwe zimekamilika.

Aidha , TFF imepewa siku TANO kujibu kama wamekubaliana na hoja hizo.


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU