Watazamaji
7,412 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga
na Toto Africans lililochezwa jana (Machi 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam na kuingiza sh. 42,508,000.
Mechi
hiyo namba 135 iliyochezeshwa na Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani
ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 45 kuibuka
na ushindi wa bao 1-0.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 9,406,764.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 6,484,271.19.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 6,708 na kuingiza sh. 33,540,000 wakati idadi ndogo
ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki
89 na kuingiza sh. 1,780,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 4,783,100.82,
tiketi sh. 4,136,390, gharama za mechi sh. 2,869,860.49, Kamati ya Ligi
sh. 2,869,860.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,434,930.25 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,116,056.86.
0 maoni:
Post a Comment